MTUMISHI WA NDANI

MTUMISHI WA NDANI


Contact Seller
Report this advert

Description

MTUMISHI WA NDANI:

Mteja wetu anayeishi Arusha anahitaji mtumishi wa ndani anayeweza kumudu majuku ya kuhudumia familia katika kwa unadhifu na ueledi Sahihi.

 

Mahali: Njiro Arusha

Mshahara: 250,000.00

Kuanza: Mapema iwezekanavyo

Uwajibikaji: Utawajibika kwa Mama na Baba wa familia hii

 

Maelezo ya nafasi hii:

Lengo la nafasi hii ni kupata mtumishi wa ndani mwenye ueledi na utashi Sahihi katika kuhudumia familia ya mteja wetu.

 

Kuwajibika kutoa huduma za ndani kwa ajili ya watoto nyumbani kwa mwajiri na majukumu yote ya msingi yanayolenga kuwahudumia watoto. Kuhakikisha usalama, malezi Sahihi na kuhakikisha Mazingira Sahihi kwa watoto kuishi na kukuwa. Utawajibika pia utahusu shughuli za nyumbani zinatekelezwa ipasavyo.

 

Majukumu:

v  Kuandaa chupa/vyombo vya watoto kulia chakula

v  Kuwabadilishia watoto nguo

v  Kuwaogesha watoto

v  Kusimamia motto mkubwa aoge

v  Kuwavalisha watoto nguo Sahihi kutokana na shughuli walioandaliwa.

v   Kuosha na kunyoosha nguo za watoto

v  Kupangilia mlo kwa ajili ya watoto kwa kushirikiana na watoto

v  Kusimamia watoto wanapokula chakula

v  Kuwafanyia usafi watoto kabla na baada ya kula chakula

v  Kufanya manununzi ya mahitaji ya watoto

v  Kupangana kusimamia shughuli mbalimbali za watoto

v  Kuwasindikiza watoto kupanda basi la shule

v  Kupanga shughuli za kimichezo zinazoweza kuwapa watoto ubunifu

v  Kuwasimamia watoto wafanye majukumu ya kishule kwa kushirikiana na wazazi

v  Kuwapeleka watoto kucheza michezo mbalimbali iliyo sahihi kwa watoto

v  Kupanga na kusimamia ratiba ya kupumzika ya watoto

v  Kusoma Pamoja na watoto wanapokuwa wanafanya kazi za shule nyumbani.

v  Kufanya usafi katika Vyumba vya watoto na kufanya usafi wa vitanda

v  Kusimamia nidhamu ya watoto ipasavyo

v  Kusimamia ratiba za kila siku za watoto

v  Kuwashirikisha watoto katika shughuli ndogondogo za nyumbani

v  Kufanya manunuzi ya watoto

 

Elimu na Udhoefu:

v  Elimu ya sekondari

v  Kama ana Mafunzo maalumu ya kutunzwa watoto ni faida zaidi

v  Ujuzi wa huduma ya kwanza na uangalizi wa watoto

v  Awe na uelewa wa usalama majumbani na ufahamu wa vyombo vya umeme

v  Ufahamu wa maeneo mbalimbali ya mji wa Arusha

v  Awe ameshafanya kazi katika familia yenye watoto wa wawili au zaidi kwa muda usiopunguwa miaka mitatu

 

Uwezo unaohitajika:

v  Mwenye utayari wa kubadilika

v  Mwenye kuzoea Mazingira mapya mapema

v  Uwezo wa kufanya majuku mengi kwa wakati mmoja

v  Utuu uzima wa kuweza kukubaliana na hali mbalimbali

v  Uwezo mzuri wa kufanya maamuzi

v  Uwezo wa kupanga na kusimamia mipango

v  Utimamu wa mwili imara

 

Namna ya kuomba:

Tuma maombi kwa barua pepe: application@expertconsultancy.co.tz . Piga simu +255759261468 na umuulizie Ismael.

 

Zingatia:

Kabla ya kupiga simu hakikisha umeelewa tangazo.

Image Gallery

Map Location