
Description
NAFASI YA MFANYAKAZI ZA NYUMBANI
Familia ya Kitanzania ya mteja wetu inahitaji mtumishi wa ndani mapema iwezekanavyo.
Familia ya wateja wetu ina makazi Njiro kwa msola na inapendelea kuwa na mtumishi wa ndani anayeweza kuishia pamoja na familia.
MASHARTI YA MSINGI:
v Lazima awapende watoto ( Umri wa watoto 6, 12 na 15/Wawili wapo shule ya kulala)
v Anayejali muda na muwajibikaji
v Lazima awe mwaminifu
v Lazima awe mcha Mungu
v Lazima awe na busara na Lugha nzuri na ya staha
MAJUKUMU ATAKAYOFANYA:
v Kusafisha maeneo yote ya nyumba (Vyombo na Vifaa vyote vya ndani)
v Kupika Vyakula mbalimbali
v Kutoa taarifa ya upungufu au kuisha kwa mahitaji ya nyumbani
v Kuangalia stoku ya mahitaji ya ndani
v Kutunza Vifaa vyote vya Usafi na kuhakikisha vipo katika hali ya usafi
v Kuhakikisha usalama wa Vyakula vinavyoandaliwa nyumbani
v Kuhakikisha watoto wanapata mahitaji yote ya msingi nyumbani
VIGENZO VINAVYOHITAJIKA:
v Uzoefu wa kazi za ndani kwa muda wa miaka 5
v Uwezo wa kujiongoza na kujihamasisha
v Muhimu kuwa na lugha ya staha na nzuri
v Awe anajua Kuweka mipango na Kuweka kipaumbele
v Msikivu anapopewa maelezo
v Awe anaungumza Kiswaili fasaha
v Elimu ya Kidato cha nne tuu
v Awe amepitia mafunzo maalumu ya utunzaji nyumba (House Keeping)
MALIPO:
v Mshahara: Tshs 250,000.00 baada ya makato yote
MASLAHI MENGINE:
v Mahali safi na salama pa kulala
v Chakula
v Nauli anapokwenda likizo na Mapumziko ya wiki
ZINGATIA:
v Waombaji waliopo Arusha watapewa kipaumbele
NAMNA YA KUTUMA MAOMBI YAKO:
Unaweza Kutuma barua ya maombi na wasifu wako kwa barua pepe hii: appli…@expertconsultancy.co.tz au unaweza kutupigia simu kwa namba hii +255747647341 (Piga muda wa kazi tuu Saa 2 asubuhi mpaka saa 10 na nusu jioni).
Image Gallery
No images.