NAFASI ZA KAZI – Moshono & King’ori – Arusha

NAFASI ZA KAZI – Moshono & King’ori – Arusha


Contact Seller
Report this advert

Description

Planet Lodges, kampuni inayoendesha “Lodges” za kitalii Moshono na karibu na uwanja wa ndege wa Kilimanjaro, King’ori Arusha, inatangaza nafasi za kazi. Kampuni inanuia kuajiri wataalamu wazoefu ili kujiunga na nasi katika msimu ujao wa kitalii utakaoanza rasmi Julai. Kama unakidhi sifa zote za kazi husika, tafadhali fikisha maombi yako Arusha Planet Lodge, kwenye anuani iliyoko mwisho wa taangazo hili.  Tafadhali usipige simu kuulizia kazi!

 

1)Mapokezi – lazima uwe na uwezo wa kuongea na kuandika Kiingereza, mtazamo mkubwa na nia ya kujifunza mambo mapya. Uwe tayari kuingia kazini shift zote usiku na mchana.  (1 post Airport Planet Lodge, 2 posts Arusha Planet Lodge)

 

2)Chef  – Lazima awe mhitimu wa chuo kinachotambulika na mwenye uzoefu wa kazi wa miaka 4 au zaidi katika jiko au mgahawa unaolisha watalii wengi.  Uzoefu wa kina wa maandalizi ya chakula na salads katima mazingira safi. Wanapaswa kuwa tayari kufanya kazi asubuhi mapema sana na kuchelewa sana kmaliza kazi (night shifts.) Uzoezu wa kupika pizza kwenye jiko la kuni (brick oven) ni kigezo muhimu pia. (1 Arusha PL & 1 post Airport PL)

 

3) Wahudumu wa Restaurant & Bar  – Awe na sifa na uzoefu wa miaka 2 kama mfanyakazi katika hoteli au mgahawa uanohudumia watalii.  Awe na uwezo wa kuelezea aina tofauti za vyakula na vilivyomoili kukidhi mahitaji ya wateja wenye mahitaji maalum. Bar – Uzoefu wa kina na ubunifu katika kuandaa aina tofauti za vinywaji hasa kahawa ni muhimu.  Atambue vinywaji tofauti kama mvinyo, bia na aina tofauti za vinywaji vikali. Awe tayari kufanya kazi asubuhi mapema sana na usiku kadri ya mahitaji ya wageni. (1 post – Barman 2 Posts – Waiter / 2 Posts Airport Waiter/s) 

 

4)Wahudumu wa vyumba – Awe na uzoefu wa kufanya usafi wa kina hasa ndani ya vyumba vya wageni na pia maeneo ya umma (Public Areas). Uzoefu na uwezo wa kuzungumza Kiingereza vizuri, uwezo wa kunyanyua masanduku yenye uzito wa kilogramu 23 bila usaidizi, utayari wa kufanya kazi asubuhi mapema na usiku. (2 Posts Airport PL & 2 Posts Arusha PL)

 

5)Security – Lazima awe amehitimu mafunzo ya mgambo aawe na ari ya kujifunza mambo mapya. Kuwa tayari kufanya kazi wakati wowote hasa usiku mzima (night shift).  ( 1 Post Airport PL  2 Posts Arusha PL)

 

5)Dereva & Maintanance –  Awe anaweza kuongea Kiingereza, amesomea ufundi wa aina fulani au uzoefu wa kina. Dereva awe na leseni ya udereva kwa ngazi ya “class C” na awe na uzoefu wa kufanya marekebisho ya kawaida ya mabomba, magari, umeme, generators, mfumo wa maji taka, kupaka rangi, kuziba na kufanyia maintanance vifaa na thamani tofauti za lodge.  Awe tayari kufanya kazi asubuhi mapema na usiku mwingi. (1 Post Airport PL 2 posts Arusha PL)

Mwisho wa kupokea maombi ni  Mei 26, 2018  Usaili utafanyika hadi Mei 30, 2018


Planet Lodges
Interview address: Plot 2271, Moshono Village Arusha, Tanzania. At the junction of Nelson Mandela and Lokii Roads i.e. the road to the small town of Kiserian.  Our entrace is opposite St. Monica school.

Image Gallery

No images.

Map Location