WATOA HUDUMA WAMINIFU NA WAELEDI WANAHITAJIKA

WATOA HUDUMA WAMINIFU NA WAELEDI WANAHITAJIKA


Contact Seller
Report this advert

Description

Kwa niaba ya mteja wetu anayejihusisha na huduma ya kuagizwa kwa haraka (Errand Service) tunahitaji watu wenye ujuzi ufuatao wajiandikishe katika daftari la mawasiliano ya kutafuta pindi huduma husika inapohitajika na wateja mbalimbali wa mteja wetu.

Hii siyo nafasi ya ajira ya moja kwa moja bali kwa muda mfupi pindi uhitaji unapojitokeza. Tunachohitaji ni watu waaminifu wanaojiendesha katika shughuli zao wenyewe na pindi mteja wetu atakapohitaji huduma zao kwa ajili ya kuwatumia kwa wateja wanaohitaji huduma hizo ataweza kuwapigia.

Kumbukumbu No: EC/HQ/VAC-53/2017

Malipo: Mapatano kutokana aina na ukubwa kazi

Atawajibika: Kwa mteja husika

Mahali: Maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha

Maelezo ya Huduma Husika:

Mteja wetu ni mtoa huduma na mfumo wake wa uendeshaji ni wa kuunganisha wahitaji ya huduma mbalimbali na watu Sahihi wenye ujuzi unaojitosheleza na pia wenye kuaminika. Lengo la huduma ya mteja wetu ni kuweka urahisi katika kupata huduma mbalimbali zinazohitajika katika maisha ya kila siku  haswa kwa watu wenye ratiba nyingi na ambao muda hauwatoshi kufanya kila kitu na ivyo kuhitaji usaidizi Sahihi.

HUDUMA TUNAZOHITAJI WATU KUJIANDIKISHA:

Mafundi Umeme:

Ø  Awe na ujuzi wa kuunganisha umeme kwenye vifaa mbalimbali majumbani na hata maofisini

Ø  Awe na uelewa mpana wa vifaa vya umeme vya aina mbalimbali

Mafundi wa Majiko ya umeme/Gesi:

Ø  Awe na udhoefu wa kurekebisha majiko ya aina mbalimbali ya gesi au umeme pindi yapoharibika

Mafundi ujenzi

Ø  Awe na uzoefu wa kufanya marekebisho madogo madogo ya nyumbani na kutengeneza vitu mbalimbali vinavyoweza kuhitajika na wateja kama masinki na kadhalika.

Wazibuaji wa vyoo, Chemba na kadhalika.

Ø  Awe na uelewa wa kazi hii na namna bora ya kutekeleza bila kuleta madhara ya kiafya kwake na kwa watu waliopo Karibu

Mafundi Uchomeaji:

Ø  Awe na ufahamu wa uchomeaji unaoweza kujitokeza mara kwa mara katika makazi ya watu.

Mafundi Rangi:

Ø  Awe na uwezo wa kushauri na kuchagua rangi za aina mbalimbali zinazoweza kupakwa majumbani.

Mafundi wa kubadilisha vitambaa na Muundo wa sofa/fanicha (thamani) mbalimbali majumbani

Wafanya usafi majumbani:

Ø  Awe na uwezo wa kuosha vyombo, kusafisha nyumba na Mazingira ya majumbani au ofisini

Waoshaji wa makapeti maofisini:

Ø  Awe na vifaa vya kuoshea makapeti ya aina mbalimbali

Mafundi wa kurepea nguo/Viatu:

Ø  Awe na uwezo wa kurepea nguo au viatu vya aina mbalimbali

Dobi/Munyooshaji Nguo:

Ø  Awe na uwezo wa kunyoosha nguo majumbani mwa wateja wetu bila wao kulazimika kupeleka nguo katika eneo lake la kazi

Waoshaji wa Matanki ya maji na vimiminika kwa ujumla:

Ø  Awe na uwezo wa kuosha matenki ya maji pindi anapohitajika kufanya ivyo

Madereva wa kukodishwa kwa kazi za muda mfupi: Tunahitaji madereva ambao pindi wateja wetu wanaposafiri katika maeneo yafuatayo wataweza kuwatembeza wakiwa salama na kwa usahihi mkubwa.

Ø  Anayewe anfahamu mji wa Nairobi kila mtaa

Ø  Awe anafahamu mji wa Arusha kila mtaa

Ø  Anayefahamu mji wa moshi kila mtaa

Ø  Anayefahamu mji wa Tanga kila mtaa

Ø  Anayefahamu Dar Es Salaam kila mtaa

Ø  Anayefahamu Dodoma kila mtaa

Ø  Anayefahamu Mwanza kila mtaa

Fundi wa baiskeli za watoto:

Ø  Awe na uwezo wa kuzitengenezea majumbani kwa wazazi wa watoto ikihitajika

Kinyozi anayeweza kuwanyoa wateja nyumbani:

Ø  Awe tayari kutumia vifaa vyake au vya mteja

Mafundi simu za kisasa;

Ø  Awe na ujuzi wa kuendana na simu mbalimbali za kisasa

Watengenezaji wa garden:

Ø  Awe na ujuzi mzuri wa kutengeneza na kutunza garden za aina mbalimbali na kwa bei nzuri.

Mtu anayeweza Kupruni miti:

Ø  Awe na uwezo wa kupanda na kupruni miti ya aina mbalimbali

SIFA ZA JUMLA:

Ø  Uaminifu kwa asilimia mia moja.Tutafuatilia

Ø  Udhoefu wa zaidi ya miaka mitatu

Ø  Kwa sababu huduma hzi zitakuwa majumbani au ofisini kwa wateja wetu utumiaji wa pombe hautakubalika

Ø  Ubunifu na lazima uwe na ushauri wa maana katika kazi husika

Ø  Lazima ujue mipaka ya kazi yako

TUNACHOHITAJI:

Ili kujumuishwa katika orodha ya watoa huduma tajwa hapo juu tunaomba uwe na vitu vifuatavyo.

Ø  Kitambulisho cha kura

Ø  Kitambulisho cha mkazi

Ø  Vyeti vya elimu yako katika eneo husika au udhibitisho wa kazi zako

Ø  Leseni ya udereva kwa madereva

NAMNA YA KUJIANDIKISHA:

Ø  Andika barua ya kuomba kuingiza katika lisiti ya kazi mojawapo

Ø  Andika list ya watu ambao ulishafanya kazi nao za aina unayomba na namba zao za simu

Tuma kwa email hii appli…@expertconsultancy.co.tz au piga simu 0759261468 naumuulizie Bwana Ismael. Mwisho wa kutuma maombi ni 31/10/2017.

Image Gallery

No images.

Map Location