
Description
Muda wa Kazi: Saa 2 asubuhi-12 Jioni
Majukumu ya Msingi:
Kuuzia wateja vinywaji na kepelekea wateja walioko mbali vinywaji kwa kutumia pikipiki.
TAARIFA NYINGINE:
· Mshahara: Tshs 100,000.00
· Chakula kitatolewa
· Nauli itatolewa kila siku
Majukumu Yanayohusika:
· Kuwasaidia wateja
· Kuwasiliana na wateja watoe order
· Kuwashawishi wateja kuhusu aina ya vinywaji wanavyoweza kuchukuwa
· Kuwaelekea wateja biashara ilipo na wanaweza kufikaje
· Kuagiza vinywaji kutoka kwa wasambazaji
· Kutoa huduma nzuri kwa wateja
· Usafi wa jumla wa Dukani na mazingira ya njee ya ofisi.
· Kufahamu taratibu za muhimu za kisheria na mionggozo ya Serikali katika uendeshaji wa maduka ya vinywaji.
· Kuendesha pikipiki kupelekea wateja vinywaji
· Kufanya mahesabu ya biashara iliyofanyika kila siku na kutoa taarifa
· Majukumu mengine utakayopangiwa na uongozi
· Kuandaa mahitaji ya duka ya kila siku
· Kumaliza kila jukumu kwa muda uliopangwa na kwa usahihi
· Kusimamia biashara ikuwe na kuimarika
Kinachohitajika:
· Uimara wa mwili na nguvu kiasi
· Uwezo wa kuendesha pikipiki au kujifunza kuendesha
· Uwezo wa kufanya maamuzi kwa usahihi na kwa umakini
· Uwezo wa kufanya hesabu kwa usahihi
Elimu na Ujuzi:
· Elimu ya Sekondari/Darasa la saba na mafunzo ya biashara kwa ngazi ya cheti
· Ujuzi wa kuendesha pikipiki
Jinsi ya Kuomba kazi hii:
Tuma maombi yako kupitia anuani hii ya barua pepe: application@expertconsultancy.