MOUNT MERU TOASTMASTERS CLUB COMMUNICATION AND LEADERSHIP CONFERENCE

MOUNT MERU TOASTMASTERS CLUB COMMUNICATION AND LEADERSHIP CONFERENCE


Contact Seller
Report this advert

Description

SEMINA KUBORESHA UWEZO WAKO WA MAWASILIANO NA UONGOZI ITAKAYOFANYIKA TAREHE 29/02/2020, KATIKA HOTELI YA CORRIDOR SPRING SAA 10.00 HADI SAA 12.00 JIONI

Clabu ya mawasiliano iitwayo Mount Meru Toastmasters Inapenda kuwaalika washarika wote katika warsha ya itakayokuwezesha kuboresha uwezo wako wa mawasiliano na uongozi na utendaji.

Toastmasters ni mpango ulioanzishwa mwaka 1924 ili kusaidia watu mbali mbali kuongeza uwezo wao wa kuwasiliana na kuongoza katika Nyanja mbalimbali za utendaji. Mpaka sasa mpango huu una wanachama wapatao  360,000 katika nchi 143 duniani. Kuna clabu  17,000  na mbili kati ya hizo ziko hapa jijini Arusha.

Warsha hizi hufanyika kila baada ya wiki mbili katika mwezi, Mount meru Toastmasters inafanya mikutano yake Jumamosi ya kwanza na ya tatu ya kila mwezi.

Faida utakayopata kwa kujiunga:

  • Utaboresha ujuzi na mbinu zaka za kuwasiliana.
  • Utajenga uwezo wako wa uongozi.
  • Utaweza kukua katika taaluma au fani yako na pia pia maeneo mengine kibinafsi.
  • Utakuza uwezo wako wa kuandika, kutayarisha na kutoa hotuba katika jukwaaa na kundi ambalo limeandaliwa kikujengea mazingira ya ushindi katika maeneo tajwa hapo juu.
  • Itakuwezesha kutambulika, na kuwa na nafasi nzuri katika maeneo yako ya utendaji kazini, katika jamii, serikali   kwasababu upeo wako utakuwa kwenye kiwango cha juu sana.
  • Uwezo wako wa kutambua mambo na kujiamini utaongezeka sana.

Mmoja wa Mtoa Mada siku hiyo ndiye aliyeanzisha warsha hizi hapa Tanzania, na haswa katika Jiji la Arusha. Aliamua kufanya hivyo kwasababu ya faida nyingi alizozipata ikiwa ni pamoja na kuongea katika majukwaa mbali mbali ya ndani na nje ya nchi. Kwa mfano alishiriki katika mashindano ya ya kuongea na kushika nafasi ya kwanza kati ya nchi tano za Afrika ya mashariki na pembe ya Africa. Pia alishiriki katika mashindano ya Dunia na kushika nafasi ya tatu. Ujuzi huu pia umwemwezesha Mtanzania huyu kufanya kazi katika nchi mbalimbali za ng’ambo ambapo anaishi hadi sasa.

Ili uweze kuelewa na kujifunza zaidi, kuhusu Toastmasters unakaribishwa kwenye warsha itakayofanyika siku ya Jumamosi tarehe 29/02/2020 katika hoteli ya Corridor Spring kuanzia saa 10.00 hadi saa 12.00 jioni.. Warsha hii itaendeshwa kwa lugha ya kiingereza na Kiswahili.

Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti  https://www.toastmasters.org/ au wasiliana

Oltesh Thobias 0754 266 300 au  Herman Kajiru on 0655896939

Image Gallery

No images.

Map Location